Annie na familia yake wanaenda pwani kwa likizo. Waokoaji wawili wa mawimbi wanatembelea shule ya Annie na anajifunza jinsi ya kukaa salama ufukweni. Annie anagundua kwamba bahari inabadilika. Mwanzoni anahofia mawimbi lakini baada ya kuwakuta na waokoaji wa mawimbi, na pamoja na usaidizi wa familia yake, Annie hugundua hivi karibuni furaha ya kuogelea pwani. Ujasiri wa Annie unaongezeka hadi anapopata wimbi kubwa ambalo humvuta ndani ya maji mengi zaidi. Je, atakumbuka jinsi ya kuwaambia wakoaji wa mawimbi kwamba anahitaji usaidizi? 'Annie na Mawimbi' ni kitabu juu ya jinsi ya kukaa salama pwani. Wakati unaposoma kitabu hiki utajifunza: · Waokoaji wa mawimbi wanavaa nyekundu na manjano · Unapaswa kuogelea katikati ya bendera nyekundu na manjano · Baadhi ya fukwe ni salama zaidi kuliko zingine · Kuna aina tofauti za mawimbi, baadhi yao ni salama zaidi kuliko mengine · Ikiwa unapata shida katika maji, tulia na inua mkono wako kuonyesha waokoaji wa mawimbi unahitaji msaada · Kuwa salama juani ufukweni. Vaa kofia na fulana ya kuogolea, na usisahau kupaka krimu ya kuzuia jua kabla ya kwenda nje katika juani Na... · Hupaswi kamwe kuingia ndani ya maji peke yako!
Hinweis: Dieser Artikel kann nur an eine deutsche Lieferadresse ausgeliefert werden.
Hinweis: Dieser Artikel kann nur an eine deutsche Lieferadresse ausgeliefert werden.