Matokeo ya utafiti huu yanalenga kurutubisha jinsi ufundishaji wa lugha ya pili hutekelezwa. Hiki ni kitabu chenye manufaa tele kwa walimu, wakuza mitaala, watafiti na wapenzi wa lugha ya Kiswahili. Wataalamu wa Kiswahili watafaidika kutokana na data nyingi iliyokusanywa nyanjani, data ambayo inaweza kutumika katika tafiti nyingine. Lugha ya Kimeru vilevile ni lugha ambayo haijaandikiwa sana kwa hivyo utafiti huu unaitendea haki kando na kuwafungulia watafiti milango ya kuitafitia lugha hii zaidi. Walimu nao, watapata fursa ya kufahamu sehemu katika lugha ambazo huwatatiza wanafunzi. Pia, watafaidika kutokana na mikakati mbalimbali ya kukabiliana na makosa haya ambayo imeshapendekezwa. Fauka ya hayo, suala la jinsia na elimu limeweza kuangaziwa. Kimsingi, hiki ni kitabu cha kila mwenye ari na ilhamu kuhusiana na masuala ya lugha.
Hinweis: Dieser Artikel kann nur an eine deutsche Lieferadresse ausgeliefert werden.
Hinweis: Dieser Artikel kann nur an eine deutsche Lieferadresse ausgeliefert werden.