44,99 €
inkl. MwSt.
Versandkostenfrei*
Versandfertig in über 4 Wochen
  • Gebundenes Buch

'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi' ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya iliyoandikwa na Enock Abiud Maregesi. Inazungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC) au Tume ya Dunia; na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa…mehr

Produktbeschreibung
'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi' ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya iliyoandikwa na Enock Abiud Maregesi. Inazungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC) au Tume ya Dunia; na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighafi ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya ¿ na kung¿oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifi a ya Magharibi ¿ na duniani kwa jumla. Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa Watanzania, Wakenya na Waganda ¿ na jamii nzima ya Afrika ya Mashariki inayozungumza Kiswahili ¿ na walowezi wa jamii yote ya Kiswahili duniani.
Autorenporträt
Enock Abiud Maregesi alizaliwa nchini Tanzania katika mkoa wa Mwanza mnamo mwaka 1972, Novemba 25. Alisomea teknolojia ya habari na utawala wa biashara katika Chuo Kikuu cha Wales, na uandishi wa habari na vitabu katika chuo cha fasihi ya ubunifu cha The Writers Bureau, nchini Uingereza. Alisomea pia sayansi ya roho ya Kabala katika Taasisi ya Bnei Baruch ya Petah Tikva nchini Israeli. Mnamo mwaka 2015 kitabu chake cha kwanza, Kolonia Santita: Laana ya Panthera Tigrisi, kilishinda Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika; iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Cornell cha New York, Marekani, na kampuni ya Mabati Rolling Mills ya Nairobi nchini Kenya. Anaishi jijini Dar es Salaam, Tanzania, anakojishughulisha na biashara na uandishi wa vitabu.