Nilikuwa nimeugua magonjwa mengi sana kwa miaka saba, na ilikuwa hali iliyokuwa haina suluhisho. Lakini kwa neema ya Mungu niliponywa magonjwa yangu yote na nikaanza kuishi maisha ya Kikristo. Wakati ule nikaota ndoto. Nilikuwa nataka kuwa mzee wa kanisa mzuri sana wa kusaidia maskini na wahitaji na kufanya kazi za umishenari ili niilipe ile neema ya Mungu. Lakini, Mungu akaniita niwe mchungaji na akanipa kazi ya kuhubiri injili kwa watu wote. Tangu nilipofungua kanisa mwaka wa 1982, nilifuata mfano wa makanisa ya kwanza, yaliyoanzishwa na mitume baada ya Bwana kufufuka na kupaa juu. Nilimakinikia maombi na uinjilisti. Kama matokeo yake, kuna zaidi ya washiriki 100,000 na makanisa wanachama 8,000 ulimwenguni kote ambayo yameungana na kuwa kitu kimoja na kanisa letu na kuhubiri injili duniani kote.
Hinweis: Dieser Artikel kann nur an eine deutsche Lieferadresse ausgeliefert werden.
Hinweis: Dieser Artikel kann nur an eine deutsche Lieferadresse ausgeliefert werden.