25,99 €
inkl. MwSt.
Versandkostenfrei*
Versandfertig in über 4 Wochen
payback
13 °P sammeln
  • Broschiertes Buch

Riwaya ya Mungu Hakopeshwi inaelezea maisha ya familia moja ya Unguja iliyoingia katika mitafaruku na mikasa mingi. Kila kitu huwa na chanzo na khatima; basi ni nini chanzo cha mitafaruku hiyo na khatima yake ilikuwaje? Simulizi ni juu ya baba, Bw. Ahmed, mwenye hasira kali zisizo na mipaka, aliyeongoza familia yake kwa utashi wa nafsi yake, bila kujali hisia za mkewe wala wanawe. Kumbe moyoni mwake alihifadhi siri, na hiyo siri ndiyo iliyomfanya Bw. Ahmed kuwa mkali bila kiasi, ikimsukuma azuie kurejea kwa yale yaliyomfika zamani. Lakini kivuli cha historia ya maisha yake ya nyuma hakikuacha…mehr

Produktbeschreibung
Riwaya ya Mungu Hakopeshwi inaelezea maisha ya familia moja ya Unguja iliyoingia katika mitafaruku na mikasa mingi. Kila kitu huwa na chanzo na khatima; basi ni nini chanzo cha mitafaruku hiyo na khatima yake ilikuwaje? Simulizi ni juu ya baba, Bw. Ahmed, mwenye hasira kali zisizo na mipaka, aliyeongoza familia yake kwa utashi wa nafsi yake, bila kujali hisia za mkewe wala wanawe. Kumbe moyoni mwake alihifadhi siri, na hiyo siri ndiyo iliyomfanya Bw. Ahmed kuwa mkali bila kiasi, ikimsukuma azuie kurejea kwa yale yaliyomfika zamani. Lakini kivuli cha historia ya maisha yake ya nyuma hakikuacha kumuandama. Riwaya hii i meandikwa kwa lugha nzuri na fasaha, kwa ufundi wa msanii makini na mwelewa wa maisha ya jamii za Kizanzibari na za mwambao kwa jumla.
Hinweis: Dieser Artikel kann nur an eine deutsche Lieferadresse ausgeliefert werden.
Autorenporträt
ZAINAB ALWI BAHAROON alizaliwa Mji Mkongwe, Zanzibar. Licha ya umri wake anaonesha katika riwaya hii dalili zote za kipaji cha uandishi wa riwaya, na kuwa kazi zake zitakuja kushamiri na kumpandisha kwenye jukwaa la waandishi maarufu.Hii ni riwaya yake ya mwanzo.