15,99 €
inkl. MwSt.

Versandfertig in über 4 Wochen
payback
8 °P sammeln
  • Broschiertes Buch

Ni Siku Gani ya Sabato, Jumamosi au Jumapili? Watu wengi hujiuliza juu ya 'sabato' - Je, tukusanyike siku gani kati ya jumamosi au jumapili? Sawasawa na Agano Jipya, jumapili inaitwa 'siku ya kwanza ya juma' na inafuata 'Sabato', yaani, 'jumamosi'. "Hata sabato ilipokwisha, kupambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi." (Mathayo 28:1). "Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma...". (Marko 16:9). Hii 'siku ya kwanza ya juma' ndiyo siku ambayo Bwana Yesu alifufuka kutoka wafu, ingawa ni wazi kuwa Wakristo walikuwa na desturi…mehr

Produktbeschreibung
Ni Siku Gani ya Sabato, Jumamosi au Jumapili? Watu wengi hujiuliza juu ya 'sabato' - Je, tukusanyike siku gani kati ya jumamosi au jumapili? Sawasawa na Agano Jipya, jumapili inaitwa 'siku ya kwanza ya juma' na inafuata 'Sabato', yaani, 'jumamosi'. "Hata sabato ilipokwisha, kupambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi." (Mathayo 28:1). "Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma...". (Marko 16:9). Hii 'siku ya kwanza ya juma' ndiyo siku ambayo Bwana Yesu alifufuka kutoka wafu, ingawa ni wazi kuwa Wakristo walikuwa na desturi au walianzisha desturi ya kukusanyika jumapili, yaani, 'siku ya kwanza ya juma'. Maneno haya yanadhibitishwa na mistari hii, "Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kuumega mkate, Paulo akawahutubu..." (Matendo 20:7). "Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja..." (1 Wakor.16:2). Hata hivyo, hakuna agizo katika Agano Jipya, kwamba lazima tukusanyike jumapili, lakini tunao mfano wa desturi ya Wakristo wa wakati wa mitume, na desturi hiyo inaendelea mpaka sasa. Desturi hiyo haikuanza tu karne ya tatu baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu, bali ilikuwa desturi ya waumini kuanzia mwanzo wa kanisa la Bwana! Katika Agano Jipya hamna mstari hata mmoja usemao wakristo walikusanya siku ya sabato au ilikuwa desturi yao au wala sheria ya wakristo kufanya hivyo! Kwa kweli ni jambo la kushangaza kwa sababu wengine wanadai kuwa tungekusanyika 'jumapili' - kwa Kiingereza 'Sunday' - ina maana tunaabudu sanamu, kwa sababu wanasema 'Sunday' inamaanisha siku ya 'jua'! (sun=jua; day=siku). Warumi waliiita siku hiyo kwa 'kuliheshimu' jua. Kama tulivyoona, wakristo wa wakati wa mitume walikusanyika jumapili kabla ya jina 'Sunday' halijatokea! Zaidi ya hayo watu wa mataifa pia waliita majina ya siku kwa kadiri walivyopenda. Lakini ukweli uko wazi kabisa kuwa jambo hili haliwahusu wakristo wala imani yao! Kwa Kiingereza Jumamosi inaitwa 'Saturday' ambayo inatokana na Warumi ambao waliiita siku hiyo 'Siku ya sayari Zohali' (dies Saturni) kwa sababu Warumi waliheshimu sayari Zohali. Kwa hiyo, ina maana wasabato wanaabudu sayari Zohali? Je, wasabato wanakosa kwa kuabudu sanamu? Ni jambo la kushangaa kwa sababu watu wanajadiliana mambo yasiyo na maana wala msingi wowote, kwa maneno tu yasiyo na mantiki yoyote. Lengo la somo hili ni kuonyesha hamna sheria katika Agano Jipya ambayo inatufundisha lazima tukusanye jumamosi. Kufanya hivyo ni kosa kubwa na udanganyifu. Lengo la somo hili siyo kutufundisha lazima tukusanyike jumapili. Nilinukulu mistari kuonyesha ilikuwa desturi ya wakristo kusanyika hasa jumapili. Lakini siyo sheria. Mwanzoni wakristo walikusanyika hata kila siku! Matendo ya Mitume 2:46. Ya mwisho, lengo la somo hili ni kuonyesha na kueleza tabia ya wokovu wetu ndani ya Kristo Yesu na vipi fundisho lile la kushika sabato linavyopinga lengo la Mungu kupitia Mwanawe. Ni wazi kumpenda Mungu, kumwamini, kumtii na kumabudu ni jambo la kila siku, kila wakati na kila nafasi - siyo la jumapili tu! Shimba Theological Institute Dkt. Maxwell Shimba
Hinweis: Dieser Artikel kann nur an eine deutsche Lieferadresse ausgeliefert werden.