32,99 €
inkl. MwSt.
Versandkostenfrei*
Versandfertig in über 4 Wochen
payback
16 °P sammeln
  • Broschiertes Buch

Mwanamke kama dutu la udongo wa mfinyanzi huumbwa na kuumbuliwa na jamii kwa namna mbalimbali. Kama kinyonga, uso wake unabeba rangi tofauti tofauti kulingana na mikondo ya maisha na mapigo ya wakati. Itakuwaje mwanamke awe wa kuozwa kama mwenye ugaga wa hisia za kujichagulia mwenyewe; au awe wa kuuzwa kama pakacha la maembe katika soko la umma? Uso wa mwanamke ni njia mbilimbili; ikiwa hazai analea, asipokuwa akirembesha anarembeshwa, kama hatumbuizi anatumbuizwa, ikiwa hajengi anabomoa; na kila mtu anamtazama na kumtarajia aonyeshe uongofu wa malaika kama kwamba yeye si mtu. Haya yanapokolea…mehr

Produktbeschreibung
Mwanamke kama dutu la udongo wa mfinyanzi huumbwa na kuumbuliwa na jamii kwa namna mbalimbali. Kama kinyonga, uso wake unabeba rangi tofauti tofauti kulingana na mikondo ya maisha na mapigo ya wakati. Itakuwaje mwanamke awe wa kuozwa kama mwenye ugaga wa hisia za kujichagulia mwenyewe; au awe wa kuuzwa kama pakacha la maembe katika soko la umma? Uso wa mwanamke ni njia mbilimbili; ikiwa hazai analea, asipokuwa akirembesha anarembeshwa, kama hatumbuizi anatumbuizwa, ikiwa hajengi anabomoa; na kila mtu anamtazama na kumtarajia aonyeshe uongofu wa malaika kama kwamba yeye si mtu. Haya yanapokolea ndipo mwanamke anaonyesha nyuso zake. Nana, msichana mrembo anajipata katikati ya jamii yenye mielekeo ya kumfinyanga mwanamke na kumyumbisha kama kayamba. Kila anayemwona Nana anamchukulia kuwa ni pambo la mji lenye nyuso nyingi au lisilokuwa na uso hata mmoja. "...Bwana Hila... alidhani tu maisha ya mwanamke ni kustareheshwa ...anachostahiki ni kupewa kila kitu anachokitaka...apewe mawazi ya kifahari, manukato ghali, chakula cha rutuba...mradi tu mwanamke abaki ndani kungoja kumstarehesha bwana." Anapotambua kuwa ana nyuso nyingi, Nana anajitazama kwa kioo kipya na kuanza safari mpya.