Sikuelewa siri ya ndani ya majaliwa ya uumbaji wa Mungu na siri iliyofichika katika msalaba miaka kadhaa ya mwanzo wa maisha yangu ya ukristo. Baada ya kuitwa kuwa mtumishi wa injili, nilianza kujiuliza, "Ninawezaje kuwaongoza watu katika njia ya wokovu na nikamtukuza Mungu?" Nikatambua kuwa ninapaswa kuielewa Biblia ikiwa ni pamoja na vifungu vigumu kuvielewa kwa msaada wa Mungu mwenyewe na kuvihubiri ulimwenguni kote. Nilifunga na kuliombea hili mara nyingi kadri nilivyoweza. Miaka saba ilipita kabla Mungu hajaanza kunifunulia.
Hinweis: Dieser Artikel kann nur an eine deutsche Lieferadresse ausgeliefert werden.
Hinweis: Dieser Artikel kann nur an eine deutsche Lieferadresse ausgeliefert werden.