Hiki ni kitabu ambacho ni msaada mkubwa sana kwa waamini, kwani kinatoa funguo muhimu na kweli muhimu zitakazomsaidia mwamini kukua katika kumjua Mungu. Kimejawa na miongozo mingi yenye kufaa katika mazingira halisi na ya kimaandiko, inayohusu ukuaji wa kiroho wa mwamini. Masomo yaliyotajwa hapo chini yametazamwa kwa upana:
- Nini maana ya kuokolewa
- Umuhimu wa Neno la Mungu
- Ubatizo wa maji, agizo
- Maombi, kipaumbele
- Umuhimu wa ushirika
- Umuhimu wa neema ya Mungu
- Ukombozi kutoka katika vifungo
- Kujawa na Roho Mtakatifu