Liv Lokke anafanya kazi kwenye duka la jumla la Netto lililoko Paderup, kama mhudumu katika eneo la kulipia. Anachukia mji huo, yeye mwenyewe, kazi yake, na maisha yake yasiyo na umuhimu; na hata hana haja ya kuwaangalia wanunuzi kujua ni akina nani. Anajua watu wengi kwenye eneo hilo na mitindo yao ya ununuzi. Lakini siku moja, inambidi amwangalie mteja fulani aliyenunua bidhaa ambayo ilimkumbusha maisha yaliyopita, na siku ile yenye mkasa ambapo alimuokoa kaka yake kutoka kwa nyumba iliyokuwa ikiteketea moto, baada ya mlipuko wa gesi kumuua mamake. Ni yeye... mpenzi wa mamake. Anadai kuwa na ushahidi kuwa kifo cha mama yake hakikuwa ajali.
Dieser Download kann aus rechtlichen Gründen nur mit Rechnungsadresse in A, B, BG, CY, CZ, D, DK, EW, E, FIN, F, GR, HR, H, IRL, I, LT, L, LR, M, NL, PL, P, R, S, SLO, SK ausgeliefert werden.