Maisha ni safari ya kulitafuta na kulifikia kusudi la uwepo wetu katika sayari ya dunia. Mafanikio ni matokeo ya kuishi na kutembea katika kusudi la uwepo wetu hapa duniani. Kulitambua kusudi hilo ndilo jambo la kwanza lakini jambo la pili ni kuzifahamu kanuni za siri zinazowaongoza wanadamu kulifikia kusudi. Kutokuzifahamu kanuni hizo hufanya watu wengi kuyaendea maisha kwa mashaka bila kuwa na uelekeo maalum huku wakijitaabisha kila siku bila mafanikio.
Hii ni kwa sababu mafanikio ya mwanadamu katika eneo lolote la maisha ni sayansi yenye kanuni maalum na thabiti zizizo na makosa ambazo hufanya kazi pale mtu anapozitumia kwa kujua ama pasipo kujua. Watu wengi wamezitumia kanuni hizi bila kujua na kuwapelekea kupiga hatua kubwa kimaisha. Wapo ambao wanazijua kanuni hizi na wamezitumia kufanikiwa katika maeneo mbali mbali waliyoyataka.
Kama ilivyo kawaida ya kanuni, unapokosea kuitumia kanuni huwezi kupata majibu sahihi na pia unaweza kupata madhara yatokanayo na kukosea kanuni. Asilimia karibu 98 ya watu duniani hawazifahamu kanuni hizi na wengi wanafanya mambo mengi kinyume na kanuni na hivyo kuzidi kuishi katika maisha magumu yenye maumivu kwa sababu ya kukosa kujua kanuni hizi za asili.
Ipo kanuni moja kuu katika kanuni za asili ambayo inaongoza kanuni zote na katika kanuni hii ndipo kuna siri ya mafanikio ya wanadamu katika sayari ya dunia. Makosa ya kuitumia kanuni hii kubwa hupelekea matatizo yasiyokwisha na kukwama katika maisha ya binadamu. Cha ajabu ni kwamba kanuni hii ipo kila mahali hata katika vitabu vyote vya dini lakini ni watu wachache sana wanaoifahamu. Yaani ni kama asilimia moja au mbili hivi ya watu huifahamu kanuni hii na namna inavyofanya kazi. Mara nyingi kanuni hii imefanywa siri kutokana na kwamba akili za watu wengi hazijafikia kiwango cha kuielewa na pia wengi wanaoijua huamini kwamba kanuni hii hujifunua tu pale ambapo mtu anakua na kiu au shauku kubwa ya ndani ya kutaka kuifahamu au kufahamu chanzo cha mambo.
Kanuni hii ya siri sasa ipo mikononi mwako, ni jukumu lako kuanza kuitumia na kuchukua hatua kurekebisha makosa na kuitumia kujiletea mafanikio binafsi na yale yatakayoigusa jamii yako na taifa lako. Hii ni siri yenye nguvu za ajabu na ninaamini utakapomaliza kukisoma kitabu hiki hutabaki kama vile ulivyokua mwanzo.

Dieser Download kann aus rechtlichen Gründen nur mit Rechnungsadresse in A, B, CY, CZ, D, DK, EW, E, FIN, F, GR, H, IRL, I, LT, L, LR, M, NL, PL, P, R, S, SLO, SK ausgeliefert werden.