Mmoja ilielezwa alifikwa na ajali akiwa mafichoni mbugani alipofika kama mtalii. Mwingine ikitajwa alikuwa akikimbia kuelekea kujificha, ndiyo hapo alifikwa na mauti akiwa njiani. Ikawa habari iliyoshika hisia za wengi, kiasi cha kuibua wanaharakati na watu wa mitandaoni baada ya kuachiwa makala toka kwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi.
Suala hilo lilimvutia Norbert Kaila baada ya kuona lilikuwa likihusu ubadhirifu, alitaka kufanya utafiti na kuweka kila kitu wazi. Alipoingia kwenye kazi hiyo, ndiyo hapo alikuja kukutana na mengine ambayo hakuyajua. Mchezo mchafu ukihusisha mfanyabiashara na watumishi wa taasisi zile za wafanyakazi wale.
Dieser Download kann aus rechtlichen Gründen nur mit Rechnungsadresse in A, B, CY, CZ, D, DK, EW, E, FIN, F, GR, H, IRL, I, LT, L, LR, M, NL, PL, P, R, S, SLO, SK ausgeliefert werden.