7,99 €
7,99 €
inkl. MwSt.
Sofort per Download lieferbar
payback
0 °P sammeln
7,99 €
7,99 €
inkl. MwSt.
Sofort per Download lieferbar

Alle Infos zum eBook verschenken
payback
0 °P sammeln
Als Download kaufen
7,99 €
inkl. MwSt.
Sofort per Download lieferbar
payback
0 °P sammeln
Jetzt verschenken
7,99 €
inkl. MwSt.
Sofort per Download lieferbar

Alle Infos zum eBook verschenken
payback
0 °P sammeln
  • Format: ePub

Kitabu hiki kimewakusudia wale wote wanaotaka kujua mizizi ya dini ya uislamu. Kimejengwa katika Sura kuu nne ambazo asili yake zinachochea udadisi na kiu ya watu kuchimba zaidi na kuja na maarifa yanayoweza kuwakomboa wanaadamu katika karne ya ishirini na moja (21). Kitabu hiki kitawanufaisha zaidi watafiti na wanafunzi wanaoamini katika nguvu ya hoja katika kuyaendea maarifa na mada zilizojadiliwa kwa mwangaza wa vitabu vya dini. Kitabu hiki pia ni kizuri kwa wale wajiitao 'watu wasiokuwa na Imani ya dini' na hata wapinzani wa uislamu.
Sura ya Kwanza imejadili kwa mapana hoja na maswali
…mehr

  • Geräte: eReader
  • mit Kopierschutz
  • eBook Hilfe
  • Größe: 0.29MB
  • FamilySharing(5)
Produktbeschreibung
Kitabu hiki kimewakusudia wale wote wanaotaka kujua mizizi ya dini ya uislamu. Kimejengwa katika Sura kuu nne ambazo asili yake zinachochea udadisi na kiu ya watu kuchimba zaidi na kuja na maarifa yanayoweza kuwakomboa wanaadamu katika karne ya ishirini na moja (21). Kitabu hiki kitawanufaisha zaidi watafiti na wanafunzi wanaoamini katika nguvu ya hoja katika kuyaendea maarifa na mada zilizojadiliwa kwa mwangaza wa vitabu vya dini. Kitabu hiki pia ni kizuri kwa wale wajiitao 'watu wasiokuwa na Imani ya dini' na hata wapinzani wa uislamu.

Sura ya Kwanza imejadili kwa mapana hoja na maswali ya msingi kuhusu utukufu wa Kitabu cha Qur'an. Imeangazia kwa kina madai na hoja mbalimbali za kuthibitisha ama kukanusha kuwa Qur'an imetoka kwa Mwenyezi Mungu. Aidha sura hiyo pia imeangazia masuala mengine yenye mahusiano na suala hilo kuu. Mfano imejadili kwa kina nafasi ya usalama wa maandiko ya Qur'an na mwisho imejikita kuangalia kuwa Je Mwongozo wa Kitabu cha Qur'an haupitwi na wakati? Je Mwongozo huo unawahusu watu wote wa zama zote hata wanaoishi katika jamii mseto ya karne ya 21?

Sura ya pili imejengwa katika msingi wa kufahamu maana pana ya uislamu. Itamstaajabisha msomaji kubaini kuwa kiasili Wakristo na Wayahudi pia ni Waislamu. Swali linabaki kwanini kuna migongano na mivutano mingi kwa watu wenye dini moja? Sura hii inaenda mbali zaidi kwa kuangazia aina tofauti za uislamu na waislamu kwa kiwango ambacho msomaji atabainikiwa kuwa hata miongoni mwa wale wanaojiita Waumini wamo Makafiri na kinyume chake. Kwa mujibu wa Qur'an, mada hii imebainisha msingi wa Imani na kufaulu kwa mwanaadamu kwa maelezo mepesi na yenye mantiki.

Sura ya Tatu imejikita zaidi katika eneo tete ambalo wanazuoni wengi wamelijadili kimakosa na kwa kufuata madhehebu yao. Wamezikimbia hoja za Kiqur'an. Sura inabainisha nafasi ya Mitume na Manabii na tofauti zao kwa kina na kwa ushahidi wa maandiko. Zaidi ya hapo sura inatafakari dhana ya Utume kwa viumbe na jinsia mbalimbali. Hoja za msingi zimejadiliwa kwa kina kuhusu utume wa Mtume Muhammad (SAW) na kitabu kimetoa majibu ya 'hoja ya ukomo wa unabii na utume' na pia kumefafanuliwa mipaka ya hoja ya kila watu kupelekewa mtume wao.

Sura ya Nne inachokoza fikra za watu kumtazama Mtume Muhammad (SAW) kwa jicho la Qur'an. Maelezo ya msingi kuhusu sifa zake na tabia zake yametolewa kwa ushahidi wa aya za Qur'an. Tumepiga hatua moja mbele kujaribu kulinganisha na kutofautisha maelezo ndani ya Qur'an na Mtume Muhammad (SAW) kama anavyojulikana na watu wengi wanaofuata kwa kiwango kikubwa maelezo nje ya Qur'an. Sifa nyingi anazonasibishwa nazo sio zile alizopewa na Mola wake. Kwanini hali hii iko hivyo? Je kutakuwa na usalama kwa kizazi kumfuata Mtume wasiomjua kwa uhakika mwenendo wake? Je unaufahamu mstari unaotenganisha "shirk" (Ushirikina) na "kufr" (kufuru)?. Kitabu hiki kitakupatia mwangaza tofauti.


Dieser Download kann aus rechtlichen Gründen nur mit Rechnungsadresse in A, B, CY, CZ, D, DK, EW, E, FIN, F, GR, H, IRL, I, LT, L, LR, M, NL, PL, P, R, S, SLO, SK ausgeliefert werden.