Mpango wa Ukombozi unaonyeshwa kama matokeo ya kuhakikisha uhitaji wa Mungu YAHWEH kuwa na familia unakamilika. Na hili lilijulikana na kupangwa kabla ya uanguko wa mtu duniani. Hivyo tokea ufahamu huu, tunachungua kwa kina Tafsiri na Asili ya Uasi na Dhambi, na hususani Kudanganywa kwa Havaa (Eva) na Uafiki wa Adam. Kuhitimisha haya yote tunafanyia uhakiki Dhana ya Dhambi ya Asili. Pamoja na haya ni mengi mengine ya kushangaza na kustaajabisha kuhusu Uumbaji wa Mtu.
Katika haya tunajibu sababu ya uwepo wako hapa duniani, na maalumu kabisa ni yapi ndiyo wajibu na majukumu yako kama mtu. Na bila kupoteza muda tunafanyia mapitio nadharia kadhaa za uumbaji, kuthibitisha kweli ya maandiko matakatifu. Kitabu chafaa sana kwa Mafundisho ya kitaaluma.
Dieser Download kann aus rechtlichen Gründen nur mit Rechnungsadresse in A, B, CY, CZ, D, DK, EW, E, FIN, F, GR, H, IRL, I, LT, L, LR, M, NL, PL, P, R, S, SLO, SK ausgeliefert werden.