Kila mahali wananchi walibanwa, wasiangaliwe hali zao za kimaisha zipo namna gani. Mkaa wa kupikia ulianza kupigwa vita, kisa kundi la wanasiasa waliyoshirikiana na wafanyabiashara kuuza mitungi ya gesi. Waliyoishia kufanya hayo, ili watu waone mambo magumu wakimbilie huko.
Ajira nayo ikawa kitendawili, vijana wenye sifa na ufaulu mzuri wapo mtaani wakihaha huku na huko. Kisa hawana pesa ya kutoa rushwa, au mtu ambaye wanamjua kwenye mfumo. Wakaishia kujiongeza na kuwa mitaani wakifanya biashara ndogondogo.
Licha ya yote hayo baadaye miaka ya uchaguzi ikikaribia, hali inarudi kuwa nafuu kwa muda mfupi. Wale waliyolalamika na kulaani wanaishia kusifia. Wakisahau huyo aliyeshusha bei za vitu, ndiye yeye aliyeacha zipande na kuchangia.
"watu wamekuwa na akili kama za kuku, hawana kumbukumbu uwanja waliyopigwa jiwe. Wakiwekewa mtama kidogo wanaishia kuja mbio sana. Tutegemee ashinde na zaidi kwenye uchaguzi ujao. Kweli hili ni Zimwi Letu", Zumo
Dieser Download kann aus rechtlichen Gründen nur mit Rechnungsadresse in A, B, CY, CZ, D, DK, EW, E, FIN, F, GR, H, IRL, I, LT, L, LR, M, NL, PL, P, R, S, SLO, SK ausgeliefert werden.