11,99 €
inkl. MwSt.

Versandfertig in 1-2 Wochen
payback
6 °P sammeln
  • Broschiertes Buch

"Mambo 15 Tunayokosea Wakati wa Kuomba", ni kitabu kinachoeleza makosa ambayo tumekuwa tukiyafanya wakati wa kuomba yanayosababisha maombi yetu yasijibiwe na Mungu Baba. Pia, kinaeleza utofauti uliopo kati ya sala na maombi; na kina shuhuda za kweli za watu waliojibiwa maombi yao kwa kutumia mbinu ambazo Mungu Baba anataka tuzitumie wakati wa kuomba. Hakuna mtu asiyekuwa na mahitaji ya kumuomba Mungu katika maisha yake. Tunaweza kudhani kwamba: watu wenye mali nyingi, kazi nzuri, elimu kubwa, vyeo au nyadhifa fulani; hawana shida katika maisha yao. Lakini ukweli ni kwamba, kila mtu ana shida…mehr

Produktbeschreibung
"Mambo 15 Tunayokosea Wakati wa Kuomba", ni kitabu kinachoeleza makosa ambayo tumekuwa tukiyafanya wakati wa kuomba yanayosababisha maombi yetu yasijibiwe na Mungu Baba. Pia, kinaeleza utofauti uliopo kati ya sala na maombi; na kina shuhuda za kweli za watu waliojibiwa maombi yao kwa kutumia mbinu ambazo Mungu Baba anataka tuzitumie wakati wa kuomba. Hakuna mtu asiyekuwa na mahitaji ya kumuomba Mungu katika maisha yake. Tunaweza kudhani kwamba: watu wenye mali nyingi, kazi nzuri, elimu kubwa, vyeo au nyadhifa fulani; hawana shida katika maisha yao. Lakini ukweli ni kwamba, kila mtu ana shida au matatizo ambayo amekuwa akimuomba Mungu amuepushe nayo. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba: kwa nini maombi yetu yanachelewa kujibiwa au hayajibiwi kabisa na Mungu Baba? Majibu ya maswali hayo utayapata ndani ya kitabu hiki kupitia siri zilizojificha katika Maandiko Matakatifu.
Autorenporträt
Mwandishi wa kitabu hiki ni mlei wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Mt. Yakobo Mkuu Mtume-Mbande, Kigando cha Tambani; Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Ana shahada ya masomo ya lugha (B.A Language Studies) katika lugha za Kiswahili, Kifaransa na 'Linguistics' kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Amewahi kufanya kazi za: uhariri, uandishi wa vitabu, uandishi wa makala kwenye magazeti mbalimbali likiwemo Gazeti la Mwananchi, ufundishaji wa masomo ya lugha katika taasisi na makampuni mbalimbali nchini Tanzania. Kwa sasa ni mhariri wa kujitegemea wa vitabu, nyaraka mbalimbali na makala za magazetini. Pia, ni mfasiri (translator) wa lugha za Kiswahili, Kingereza na Kifaransa.