Nimeshuhudia kuna watu wanasema wana mikosi, kuna wengine wanasema hawana bahati na asilimia kubwa siyo kwamba hawajafanikiwa ila hawastahili kuwa na kiwango hiko cha mafanikio. Watu hawa endapo wakiwa tu na nguvu ya ushawishi wanaoweza kufanikiwa zaidi .
Ukweli ni kwamba USIPOJUA KUSHAWISHI WATU WAKUPE VITU BASI UWEZI PATA CHOCHOTE KUTOKA KWA WATU,
Baada ya miaka mingi ya kuwa mwandishi na mkufunzi niligundua sheria 10 za ushawishi ambazo zinaweza kutumiwa na mtu yoyote kupata chochote anachotamani kutoka kwa WATU
Inawezekana siyo kwamba hauna wateja, Ila hujui kushawishi wateja
Inawezekana siyo kwamba hakuna kazi, ila ujui kushawishi watu wakupe kazi
Inawezekana siyo kwamba hakuna kabisa watu w kukusaidia ila ujui namna gani ya kushawishi watu wakusaidie
Tatizo siyo mtaji, Tatizo unashindwa kushawishi watu wakupe mtaji.
Katika kitabu changu cha Hatua nimefundisha jinsi watu wanavyoweza kufanyika Muujiza Katika maisha yako, katika kitabu hiki nitakufundisha sheria 10 zitakazo ongeza ushawishi wako na kufanya watu wakupe chochote unachokitaka
Watu ndo mtaji wa kwanza ili uweze kupiga hatua katika maisha yako ili uweze kutoka hapo ulipo. Sijui kwa sasa una hali gani katika uchumi, katika afya,kwenye Maisha yako ya kila siku lakini kupitia kitabu hiki utaenda kupata chochote ulichokuwa unakitamani kutoka kwa watu kwa urahisi sana.
Unaposoma kitabu hiki utajifunza sheria nyingi zitakazo kufanya kuwa wa tofauti na nyuma kabisa na utakuwa imara Zaidi katika ushawishi
"Mungu akuongoze katika usomaji wa kitabu hiki"
Mwandishi/Mkufunzi&Mwamasishaji.
ERICK EBELHARD MBELEKA
Dieser Download kann aus rechtlichen Gründen nur mit Rechnungsadresse in A, B, CY, CZ, D, DK, EW, E, FIN, F, GR, H, IRL, I, LT, L, LR, M, NL, PL, P, R, S, SLO, SK ausgeliefert werden.